Siri ya Mtungi - Sehemu ya 21 (with English Subtitles)

Siri ya Mtungi - Sehemu ya 21 (with English Subtitles)

SUBSCRIBE: \rbr\rbrCheusi mara zote hukimbilia ushauri wa Mama yake kipindi anapo kuwa na msongamano wa mawazo. Lakini alipogundua kuna mwanaume alie uchi chumbani kwa Mwanaidi hiyo ndio ikawa sauti ya kumwamsha kuanza kufanya maamuzi yake mwenyewe badala ya kumtegemea mtu mwingine.\rbr\rbrDuma anajihusisha zaidi na biashara ya kusafirisha madawa ya kulevya ambayo ni ya Golden na Ishi. Hatari ni kubwa, sio kutokana na sheria tu, bali Masharubu adui mkubwa wao na hivi sasa wako vitani.\rbr\rbrMzee Kizito anajitahidi kujenga penzi upya na wake zake lakini Mwanaidi anajiweka mbali wakati Nusura amejikita kwenye ujauzito wake na Farida amedhamilia kulipiza kisasi baada ya kutelekezwa kwenye ndoa isiyo ya kimapenzi. Wanawake wote watatu wanaficha siri kubwa sana.\rbr\rbrCheche analazimishwa kuitunza ndoa alio iharibu mwenyewe. Siku Cheche anapowapiga picha za kumbukumbu ya ndoa ya kikongwe familia ya Gwerume, Cheche ana hamasishwa sana na upendo wao, mshikamano na uvumilivu wao wa muda mrefu.


User: Rosalinaogrenr

Views: 103

Uploaded: 2016-02-12

Duration: 29:50