KISA NONDO: IGP Sirro, DC1, Waitwa Mahakamani

KISA NONDO: IGP Sirro, DC1, Waitwa Mahakamani

KISA NONDO: IGP Sirro, Mambosasa, DC1 Waitwa Mahakamanibr br MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wito wa kuwaita Mkrugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kufika mahakamani kesho Jumatano, Machi 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo.br br Taarifa za wito huo umetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole ambaye ametoa taarifa hiyo fupi kupitia kwenye ukurasa wake maalum wa Twitter.br br Kambole amesema “Wito umetolewa leo (jana Machi 19) Mahakama kuu mbele ya Jaji Samejikwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani 21032018 kujibu kesi ya Abdul Nondo”.br br Kambole amesema washitakiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa Jumatano, ni IGP Simon Sirro ameitwa kwa sababu yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini hivyo vituo vyote na polisi wapo chini yake lakini bado Nondo amekuwa hapatikani katika vituo vya polisi.br br Aidha, amesema kuwa katika jalada lililofunguliwa leo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), naye kahusishwa kwa sababu mara ya mwisho Nondo alipokelewa na yeye alipofikishwa Dar es salaam kutoka Iringa na kwamba alimchukua kama muathirika wa tukio la utekwaji na siyo mshtakiwa.br br Hata hivyo Kambole amesema ameshafanya jitihada nyingi za kutaka kuonana na mteja wake lakini hadi sasa juhudi zake hazijafua dafu.br br Abdul Nondo anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Machi 7, ambapo awali aliripotiwa kupotea na kesho yake kujikuta Iringa.br br Baadaye alisafirishwa hadi Dar kwa ajili ya upelelezi zaidi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar, Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari alisema wanamshikilia Nondo kwa ajilili ya upelelezi na watakapokamilisha watamfikisha mahakamani.br br Install #GlobalPublishersApp Android: iOS: Subscribe FACEBOOK: ... br br TWITTER: Visit , Subscribe br br kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… WEBSITE: FACEBOOK: ... TWITTER: INSTAGRAM: ..


User: video bora

Views: 0

Uploaded: 2018-03-22

Duration: 02:14